Jumanne 18 Novemba 2025 - 17:09
Maduro: Kuitetea Palestina ni jukumu la kihistoria na tukufu

Hawza/ Rais wa Venezuela, katika maadhimisho ya mwaka wa kuadhimishwa kwa tangazo la uhuru wa Palestina, amesisitiza msimamo thabiti na wa kihistoria wa Caracas katika kuutetea mustakabali wa Wapalestina, akisema kwamba; bila kutendeka haki dhidi ya jinai za Israel huko Ghaza, amani ya kudumu katika eneo hilo haiwezi kupatikana.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza,Shirika la Habari la Hawza, Nicolás Maduro, Rais wa Venezuela, katika ujumbe rasmi uliotolewa katika maadhimisho ya mwaka wa 37 tangu kutangazwa kwa uhuru wa Palestina, alisisitiza juu ya kushikamana kihistoria na msaada usiotikisika wa nchi yake kwa taifa la Palestina. Alibainisha kuwa suala la Palestina si hoja ya kisiasa tu, bali ni jukumu takatifu na wito wa dhamiri hai kwa mataifa yote huru duniani.

Maduro, akirejea miongo kadhaa ya uvamizi, mzingiro na kile alichokieleza kuwa “uhalifu wa kigaidi wa kiserikali” unaofanywa dhidi ya Wapalestina, alisema: “Wapalestina wana haki ya kuishi kwa amani na kuunda dola yao huru. Tutaendelea kusimama nao hadi siku ya ukombozi kamili wa Palestina; siku ambayo itasajiliwa katika historia kama ushindi wa hadhi ya kibinadamu.”

Rais huyo wa Venezuela, akilaani vikali jinai za Israel huko Ghaza, alisisitiza: “Amani ya kweli itapatikana pale tu ambapo jumuiya ya kimataifa itailazimisha Israel kuwajibika kwa uhalifu na vitendo vya mauaji ya kimbari.” Alikosoa pia kutokuchukua hatua kwa baadhi ya serikali na akasema kwamba “nguvu ya mtazamo wa umma” ndio inayoweza kukomesha mzunguko wa mauaji na maonesho ya kinafiki ya ‘kutafuta amani’ yanayofanywa na utawala wa Kizayuni.

Maduro aliongeza kuwa utekelezaji wa haki utakua ndio njia ya kufungua milango ya ujenzi mpya wa Ghaza, na akasema: “Venezuela inaendelea kupaza sauti yake ikidai kutendeka haki kuhusu jinai za Israel.”

Katika muktadha huohuo, Ivan Gil, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, katika taarifa tofauti alisema kuwa taifa la Palestina kwa zaidi ya miaka 75 limekuwa mhanga wa uvamizi na ubaguzi wa kimfumo. Alisisitiza kuwa hatua za utawala wa Kizayuni ni uvunjaji wa wazi wa sheria za kimataifa na misingi ya Katiba ya Umoja wa Mataifa. Akasema: “Venezuela inathibitisha upya msimamo wake wa kina na thabiti wa kulisaidia taifa na serikali ya Palestina.”

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Baraza la Kitaifa la Palestina linalohusiana na Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO) lilitangaza kuundwa kwa dola huru ya Palestina mnamo mwaka 1988 huko Algeria; tamko lililotolewa kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa nambari 242 na 338, likiitaka Israel kuondoa kabisa majeshi yake ya uvamizi.

Leo, baada ya kupita miaka 37 tangu tamko hilo la uhuru, suala la Palestina bado limebaki kuwa miongoni mwa madai endelevu na thabiti, zaidi ya mataifa duniani na watu wa Palestina wanaendelea kusisitiza haki yao ya kujitawala na kujiamulia mustakabali wao wenyewe.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha